Matabibu Gaza wasema mashambulizi ya Israel yamewaua watu 23
25 Machi 2025Kwa mujibu wa hospitali ya Nasser ambayo imepokea miili mingi pamoja na majeruhi kadhaa tangu kuanza tena kwa mashambulizi ya Israel katika ukanda huo wa Gaza wiki iliyopita, waliouawa ni pamoja na watoto watatu na wazazi wao katika shambulizi dhidi ya kambi moja karibu na mji wa kusini wa Khan Younis.
Haya yanajiri wakati Israel imesema mwandishi mmoja wa habari wa shirika la Al Jazeera ameuawa Gaza kutokana na shambulizi la mlenga shabaha wa Hamas.
Wakati huo huo, mmoja wa wakurugenzi wa filamu iliyoshinda tuzo ya oscar kwa jina ''No other Land'' Hamdan Ballal, bado hajulikani alipo baada kupigwa na walowezi wa kiyahudi na kuzuiliwa na jeshi la Israel.
Wakili Lea Tsemel ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa hana taarifa kumhusu Ballal, karibu saa 12 baada ya mashahidi kusema alishambuliwa na kuzuiliwa.