Kosa la uhaini ni moja ya makosa makubwa ya jinai yanayohusisha vitendo vya mtu au kikundi cha watu vinavyolenga kuhatarisha usalama wa taifa, kuipindua serikali halali, au kushirikiana na maadui wa nchi kwa njia yoyote ile. Adhabu yake ni kunyongwa, na inatekelezeka katika mataifa yaliyosaini mkataba wa Roma. Tunaliangazia kosa la uhaini katika nchi za Afrika Mashariki hasa tukiimulika Tanzania.