Mashirika ya misaada yaonya kuhusu usambazaji misaada Gaza
9 Mei 2025Mashirika ya misaada yametahadharisha leo kwamba mipango iliyowasilishwa na Israel kudhibiti usambazaji wa misaada huko Gaza, likiwemo pendekezo linaloungwa mkono na Marekani, utaongeza mateso na vifo katika eneo hilo la Palestina ambalo limekuwa chini ya mzingiro kamili kwa karibu wiki kumi.
Mashirika hayo yameitolea wito Israel ifute marufuku yake dhidi ya vyakula vyote, dawa na mahitaji mengine kuingia Gaza.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF James Elder amesema mjini Geneva kwamba msaada wa kibinadamu hautakiwi kutumiwa kama nyenzo ya kushinikiza mazungumzo.
Balozi wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee amesema mfumo mpya wa utoaji misaada ya kiutu na chakula Gaza utazinduliwa huku upelekaji misaada ukitarajiwa kuanza hivi karibuni.