Mashirika ya misaada yataka ugavi wa msaada Gaza ufutwe
1 Julai 2025Matangazo
Zaidi ya mashirika 170 ya misaada na asasi zisizo za kiserikali leo wametoa wito mpango wa usambazaji chakula unaoungwa mkono na Marekani na Israel katika Ukanda wa Gaza ufutiliwe mbali kutokana na wasiwasi kwamba unawaweka raia katika hatari ya kifo na majeraha.
Mashirika hayo yamesema katika taarifa kwamba Wapalestina katika Gaza wanakabiliwa na chaguo lisilowezekana la kufa njaa au kuikabili hatari ya kupigwa risasi wakati wanapojaribu kukifikia chakula kwa ajili ya kuzilisha familia zao.
Miongoni mwa mashirika yaliyosaini taarifa hiyo ya pamoja ni Oxfam, Madaktari wasio na mipaka, Shirika la hisani kwa watoto la Save the Children, Baraza la Wakimbizi la Norway na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International.