MigogoroSudan
Mashirika: Sudan inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinaadamu
19 Julai 2025Matangazo
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya raia 450 ikiwa ni pamoja na watoto 35, waliuawa wiki iliyopita kufuatia mashambulizi katika vijiji vilivyo pembezuni mwa mji wa Bara katika mkoa wa Kordofan Kaskazini.
Sudan ilitumbukia katika vita mwezi April mwaka 2023 baada ya mvutano mkali kuibuka kati ya jeshi na vikosi vya RSF. Ghasia hizo zimesababisha vifo vya watu wasiopungua 40,000 na kusababisha njaa na mgogoro mkubwa wa kibinaadamu ambapo inakadiriwa kuwa watu milioni 13 wamegeuka kuwa wakimbizi.