Mashirika ya kiraia yauomba Umoja wa Afrika kuidhibiti Mali
14 Februari 2025Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch siku ya Alhamisi liliutaka Umoja wa Afrika kuchukua hatua za haraka dhidi ya serikali ya Mali ili kukomesha ukandamizaji kwa wapinzani nchini humo.
Taifa hilo la Afrika Magharibi, linaloongozwa na jeshi tangu mapinduzi mawili mfululizo mwaka 2020 na 2021, limekuwa likishutumiwa mara kwa mara kwa kujaribu kunyamazisha ukosoaji.
Soma pia: Duru za usalama: Watu zaidi ya 70 waliuawa katika shambulio la Bamako
Katika barua yake kwa Tume ya Afŕika ya Haki za Binadamu na Watu, shirika hilo limesema karibu watu 11 wanazuiliwa hadi sasa "kwa sababu za kisiasa", ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa upinzani.
Amesema, tangu mapinduzi ya kijeshi, serikali ya Mali imeongeza mbinyo dhidi ya wapinzani wa kisiasa, mashirika ya kiraia na vyombo vya habari, na kupunguza nafasi ya raia kwenye siasa ya nchi.