JamiiAsia
Mashirika yataka misaada zaidi ya kiutu kwa Afghanistan
4 Septemba 2025Matangazo
Mashirika ya misaada yataka jamii ya kimataifa kuongeza ufadhili kwa Afghanistan baada ya tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha richter 6.0 kuua angalau watu 1,400 na kuwajeruhi maelfu wengine. Uingereza imetoa msaada wa dola milioni 1.3, ambapo fedha hizo zitaelekezwa kwa mashirika ya misaada na si kwa serikali ya Taliban, ambayo Uingereza haijaitambua rasmi. Korea Kusini siku ya Jumatano ilitangaza kuwa itatoa dola milioni 1 kupitia Umoja wa Mataifa.Tetemeko hilo lilitokea usiku wa Jumapili na kuathiri majimbo kadhaa ya mashariki ya Afghanistan yenye milima na yaliyo mbali. Hili ni janga la hivi karibuni kuikumba Afghanistan, na ni tetemeko la tatu kubwa tangu kundi la Taliban lilipochukua madaraka mwaka 2021.