Mashindano ya majaribio ya riadha yafanyika Kenya
22 Julai 2025Matangazo
Kenya inaanda hivi leo mashindano ya majaribio ya wanariadha watakaoshiriki mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika mjini Tokyo nchini Japan kuanzia Septemba 13 hadi 23.
Majaribio hayo ya wanariadha yanafanyika chini ya kiwingu cha kuibuka tena wasiwasi kuhusu matumizi ya dawa za kutitimua misuli, baada ya bingwa wa kike wa mashindano ya riadha duniani, Ruth Chepngetich, kusimamishwa kwa muda kushiriki wiki iliyopita.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 alithibitika kutumia dawa za kutitimua misuli mwezi Machi kwa mujibu wa kitengo cha maadili cha Riadha. Kisa cha mwanariadha huyo pia kimezusha wasiwasi kuhusu maandalizi ya Kenya katika mashindano hayo yajayo huko mjini Tokyo.