MigogoroUlaya
Mashambulizi ya Urusi yawauwa watu 15 Ukraine
17 Juni 2025Matangazo
Maafisa wa Kyiv wamesema watu wengine 99 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo katika mji mkuu pekee.
Soma zaidi:Urusi yaifunika Ukraine kwa usiku mwengine wa droni
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameyalaani mashambulizi ya Urusi na kuyataja kuwa ya kutisha zaidi dhidi ya mji mkuu Kyiv. Amefafanua kuwa katika mashambulizi hayo, Urusi ilirusha zaidi ya droni 440 na makombora 32.