MigogoroUlaya
Mashambulizi ya Urusi yaua watu watatu huko Sumy
24 Juni 2025Matangazo
Hayo yameelezwa na mkuu wa vikosi vya jeshi wa jimbo hilo la Sumy Oleg Grygorov, akisisitiza kuwa watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Wakati huohuo, Meya wa jiji la Moscow Sergei Sobyanin amesema mapema Jumanne kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ilidungua droni mbili za Ukraine zilizokuwa zimeelekezwa katika mji mkuu huo wa Urusi, huku droni zingine zikiharibiwa huko Kursk and Bryansk.