MigogoroUlaya
Mashambulizi ya Urusi yawaua wafungwa 17 gerezani Ukraine
29 Julai 2025Matangazo
Gavana Ivan Fedorov kupitia ukurasa wake wa Telegram amesema mashambulizi ya Urusi yamesababisha uharibifu wa majengo kadhaa ndani ya gereza hilo. Ameongeza kuwa maeneo mengine jirani yalishambuliwa mara nane na baadhi ya makaazi jirani na gereza lililoshambuliwa yameathiriwa.
Kamishana wa haki za binadamu katika bunge la Ukraine Dmytro Lubinets ameeleza kuwa mashambulizi hayo ni ushahidi mwingine wa uhalifu wa kivita unaofanywa na Urusi. Amesema watu wanaoshikiliwa katika sehemu kama magereza hawajapoteza haki yao ya kuishi na kulindwa.