Mashambulizi ya Israel yawauwa watu 22 Gaza City
24 Aprili 2025Matangazo
Kulingana na taarifa ya hospitali walikopelekwa majeruhi, watu tisa waliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kituo cha zamani cha polisi huko Jabalia kaskazini mwa Gaza City, kushambuliwa na kombora.
Jeshi la Israel limesema limeshambulia kituo cha kamandi ya Hamas katika eneo la Jabalia ila halikusema iwapo lilikuwa linakilenga kituo hicho cha polisi.
Kwengineko watu watano wamefariki baada ya mahema waliyokuwamo ndani kushambuliwa na wengine wawili kuaga dunia baada ya nyumba yao kushambuliwa huko Khan Yunis.