Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni na makombora
6 Aprili 2025Idara hiyo imesema droni 53 kati ya 109 zilizorushwa zilipoteza mwelekeo. Taarifa hiyo imetolewa muda mfupi baada ya Urusi kukiri kuwa imefanya mashambulizi ya makombora dhidi ya Ukraine yaliyolenga maeneo kadhaa ukiwemo mji mkuu Kyiv.
Gazeti la mtandaoni la Kyiv Independent limemnukuu Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko akisema watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na maporomoko ya majengo yaliyolengwa wakati wa mashambulizi hayo.
Soma zaidi: Urusi, Ukraine zaendelea kushambuliana kwa makombora
Katika hatua nyingine, Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema imezidungua droni 11 za Ukraine zilizorushwa usiku wa kuamkia Jumapili. Mikoa ya Kursk na Belgorod ni miongoni mwa sehemu droni hizo zilipozuiwa. Kaimu Gavana wa eneo la Rostov amesema hakuna majeruhi waliotokana na mashambulizi hayo lakini baadhi ya majengo ya utawala yameathiriwa.