MigogoroUlaya
Urusi na Ukraine zashambuliana kwa droni, makombora
3 Mei 2025Matangazo
Kutokana na mashambulizi hayo watu 47 wamejeruhiwa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine wa Kharkiv. Meya wa mji huo Ihor Terekhov amesema droni zilishambulia maeneo 12 ya mji huo Ijumaa jioni na kuharibu pia makaazi ya watu, miundombinu na magari kadhaa.
Soma zaidi: Urusi na Ukraine zashutumiana mashambulizi ya droni
Kwa upande wake Urusi kupitia Wizara yake ya Ulinzi imesema imezidungua droni 170 za Ukraine usiku wa kuamkia Jumamosi. Mifumo yake ya ulinzi ilifanikiwa pia kuyazuia makombora kumi na moja. Watu watano wamejeruhiwa katika mji wa bandari wa Novorossiysk wakiwemo wanatoto wawili. Meya wa eneo hilo ametangaza hali ya hatari kutokana na mashambulizi hayo.