Mashambulizi ya Israel yasababisha vifo vya watu 5 Gaza
8 Mei 2025Hayo yameelezwa na Shirika la ulinzi wa kiraia katika ardhi hiyo ya Palestina.
Hayo yanajiri wakati kundi la wataalam zaidi ya 20 wa Umoja wa Mataifa wamesema viongozi wa dunia wanatakiwa kuamua kati ya "kusalia kimya na kushuhudia mauaji ya watu wasio na hatia au washiriki katika kutafuta suluhu ya haki" katika mzozo huo wa Mashariki ya Kati.
Soma pia: Hamas yasisitiza makubaliano 'ya kina' kumaliza vita Gaza
Wataalam hao wameutoa wito huo baada ya waokoaji huko Gaza kusema kuwa mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Israel jana Jumatano yamesababisha vifo vya watu 59. Wakati huohuo, Israel imesema itaitendea Iran kile ilichokifanya kwa Hamas huko Gaza, ikiwa ni siku chache baada ya shambulio kwenye uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv lililofanywa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.