Israel imeanzisha wimbi jipya la mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300, DW imetaka kufahamu mashambulizi haya mapya ya Israel huko Gaza, yanatoa picha gani katika mzozo huo? Hilo ni miongoni mwa maswali ambayo Bakari Ubena amemuuliza mchambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati, Abdel Fattah Mussa akiwa mjini Tehran.