MigogoroUlaya
Urusi yafanya mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya Ukraine
4 Julai 2025Matangazo
Zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo yaliyoulenga mji mkuu, Kyiv ambayo pia yamesababisha uharibifu wa mali na majengo likiwemo jengo ulipo ubalozi wa Poland. Kulingana na taarifa ya mamlaka za Ukraine, droni nyingi kati ya zilizorushwa ni aina ya Shahed na jumla ya makombora 11 yalirushwa na Urusi.
Wakati huohuo, mashirika ya intelijensia ya Uholanzi na Ujerumani yamebainisha kuwa yamekusanya ushahidi unaoonesha kuwa, Urusi kwa kiasi kikubwa imeongeza matumizi ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku katika vita vyake na Ukraine. Kutokana na hilo, Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Ruben Brekelmans ametoa wito wa kuiwekea Moscow vikwazo vikali zaidi.