Mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari yaongezeka
5 Machi 2025Matangazo
Ripoti hiyo iliyoidhinishwa na shirika linalofuatilia masuala ya haki za binadamu hapa Ulaya, inaonyesha idadi ya vitendo hivyo iliongezeka kutoka 26 hadi 78 mwaka jana.
Nchini Ukraine, wanahabari 19 walishambuliwa. Na idadi inahusishwa na uvamizi wa Urusi. Georgia, Serbia na Uturuki zinafuatia kwa kuwa na mashambulizi manane kila moja.
Kulingana na ripoti hiyo, hali ya wanahabari nchini Georgia ni mbaya zaidi kuliko katika nchi nyingine yoyote mwanachama wa EU, huku mashambulizi mengi yakitokea wakati wa maandamano ya kupinga sheria tata na mivutano kuhusu msimamo wa nchi hiyo kuelekea Umoja wa Ulaya.