MASHAMBULIO YAENDELEA IRAQ:
21 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq,mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Kimarekani na wanasiasa wanaoiunga mkono Marekani hayaonyeshi dalili ya kupunguka.Katika mripuko wa bomu uliotokea kwenye kijiji cha Ramadi mwanajeshi mmoja wa Kimarekani ameuawa.Wanajeshi wengine wawili walijeruhiwa baada ya mlolongo wa magari yao kushambuliwa.Na katika shambulio la kujitolea mhanga maisha,si chini ya watu watano wamefariki baada ya gari kuripuka nje ya ofisi za vyama vikuu viwili vya kisiasa vya Wakurd katika mji wa Kirkuk kaskazini mwa Iraq.Tangu rais George W.Bush wa Marekani kutangaza rasmi kuwa vita vimemalizika nchini Iraq,idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliofariki ni 180.