Mashambulio ya kujitolea mhanga yautikisa mji wa Kandahar,Afghanistan
23 Julai 2006Matangazo
Visa viwili vya mashambulio ya kujitolea mhanga viliutikisa mji muhimu wa Kusini mwa Afghanistan, Kandahar, na kuwauwa wanajeshi wawili wa jeshi la muungano. Maafisa wa serekali ya Afghanistan na mjaeshi la kimataifa linaloongozwa na Marekani walisema raia 27 wa Ki-Afghanistan na wanajeshi wanane wa jeshi la muungano pia walijeruhiwa katika miripuko iliotokea mita 100 baina ya mahala hapo pawili. Vuguvugu la Taliban lilidai dhamana ya mashambulio hayo yote mawili. Karibu ya wanajeshi wa kigeni 60 wameuwawa katika mapigano mnamo mwaka huu huko Afghanistan.