Mashambulio mapya ya Israel yauwa 22 Gaza
14 Julai 2025Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limesema mashambulizi ya anga ya Israel, yaliyofanywa hivi leo Jumatatu yameuwa takriban watu 22 huku mapigano kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo Wakipalestina wa jeshi la wapiganaji la Al Quds yakiripotiwa kaskazini mwa Ukanda huo.
Wanamgambo hao wanaowasaidia Hamas,wamechapisha video leo Jumatatu ikiwaonesha wakifyetua makombora dhidi ya kamandi na vituo vya jeshi la Israel karibu na mji wa Shujaiya.
Mapigano hayo yanafanyika katika wakati kukiwa na mkwamo kwenye mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili nchini Qatar.
Msemaji wa shirika la ulinzi wa kiraia Mahmud Bassal ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Wapalestina 10 waliuwawa kwenye mashambulizi tofauti ya anga katika maeneo mbali mbali ya Gaza City huku wengine 12 wakiuliwa katika mji wa Khan Yunis.