Mashabiki wadhibitiwa kuhudhuria mechi ya Kenya na Zambia
12 Agosti 2025Hayo yametangazwa na mwenyekiti wa Kamati Andalizi ya CHAN nchini Kenya Nicolas Musonye. Hii ni baada ya mashabiki wa nyumbani kuendelea kuvamia uwanja wa michezo kabla ya mechi kuanza.
Mashabiki walivamia uwanja wa Kasarani mjini Nairobi bila tikiti katika mechi za awali zilizoihusisha Kenya huku vidio zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wakivamia eneo hilo kwa wingi.
CHAN 2024: Harambee Stars yaishangaza Moroko
Hapo jana Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), lililipiga faini Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) ya dola elfu 17,500 kufuatia usumbufu ulioshuhudiwa katika viwanja vya michezo.
Hii ni mara ya kwanza mataifa matatu ya Afrika Mashariki Kenya, Tanzania na Uganda yameandaa michuano hiyo, lakini nafasi hiyo ya kihistoria iligubikwa na ucheleweshwaji wa utayari wa viwanja vya mpira na sasa mashabiki wanaozusha vurugu.