Masambulizi ya RSF yaua 21 Sudan
19 Mei 2025Takriban raia 21 waliuawa jana Jumapili baada ya wanamgambo wa RSF kushambulia kambi ya wakimbizi wa ndani (IDP) katika eneo lililokumbwa na vita la Darfur kwa upande wa magharibi mwa nchi hiyo. Taarifa hiyo imeandikwa katika tovuti ya kibinafsi ya Darfur24.
Shambulizi lililenga kambi ya IDP ya Abu Shouk nje kidogo ya mji wa al-Fashir, ngome kuu ya mwisho ya jeshi huko Darfur, ambayo imekuwa chini ya mzingiro wa RSF kwa mwaka mmoja. Kikundi cha uokoaji cha kujitolea cha katika eneo hilo "Emergency Response Room" kilisema kwamba makombora hayo yalitua sehemu mbalimbali za kambi hiyo, likiwemo la soko.
Kambi hiyo ya Abu Shouk ni makazi ya Wasudan wengi
Kambi hiyo ya Abu Shouk ni nyumbani kwa Wasudan wengi ambao sio tu walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea, lakini pia migogoro ya hapo awali huko Darfur.
Kwingineko, kundi lisilo la kiserikali la Wanasheria wa Dharura lilishutumu jeshi na vikosi vya washirika wake kwa kuwaua raia 18 katika mji wa al-Hamadi katika jimbo la Kordofan Kusini Mei 15, Radio Dabanga yenye maskani yake mjini Amsterdam iliripoti Ijumaa. Jeshi na RSF wameshutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu tangu vita vilipozuka Aprili 2023.
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imekataa mpango wa kikosi cha RSF kuunda serikali
Katika hatua nyingine tovuti moja ya kibinafsi nchiniSudan "Sudan Tribune" imeandika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imekataa mpango wa kikosi cha RSF na washirika wake wa kuanzisha serikali nyingine pamoja na uwepo wa serikali inayotambulika na jumuiya ya kimataifa huko Sudan, ikiiita "haramu".
Kufuatia mkutano wa viongozi wa jumuiya hiyo wa nchini Iraq, Mei 17, mmoja kati ya maafsia wake waandamizi Jamal Rushidi amesema "Suala hili limo katika makubaliano ya mataifa ya Kiarab kutokana na tishio kubwa katika umoja wa Sudan."
Nikimnukuu hapa anasema "Kilichokubaliwa katika mkutano huo kinaakisi msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu kuunga mkono umoja na utulivu wa Sudan, kujitenga na migawanyiko au masuala yanayoendana na hilo ambayo yanatishia kusambaratisha serikali."
Soma zaidi:Shambulizi la kombora la RSF laua watu 14 Darfur
Wanamgambo wa RSF na makundi washirika walitia saini mkataba nchini Kenya mwezi Februari kwa lengo la kuanzisha kile walihokiita "serikali ya amani na umoja" katika maeneo wanayodhibiti. Tangazo hilo lilizua hofu ya kugawanyika kwa Sudan.
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alionya kwamba Sudan iko katika "hatua ya hatari inayotishia umoja na utulivu wake, na hivyo kuhitaji kuchukuliwa hatua za haraka ili kuhakikisha usitishaji vita na kuhifadhi mipaka ya taifa na taasisi za Sudan".