Marufuku watu kuendesha magari Baghdad yataendelea hadi kesho
19 Agosti 2006Matangazo
Marufuku dhidi ya watu kutoka na magari ili kuepukana na mashambulio ya kigaidi wakati wa ibada za washiya, yataendelea hadi kesho katika mji mkuu wa Irak-Baghdad.Watu sabaa waliuwawa jana baada ya kufyetuliwa risasi na watu waliokua ndani ya gari.Kila mwaka, maelfu ya waumini wa madhehebu ya shiya,wanakusanyika msikitini kuomboleza kifo cha Imam Musa al Kadim.Mwaka jana waumini elfu moja waliuwawa mtafaruku ulipozuka katika daraja ya Tigris,kwa dhana kuna mtu aliyejiripua karibu na hapo.