Karua: Uhuru wa watu wa Afrika Mashariki unadorora
23 Mei 2025Matangazo
Karua amewatuhumu viongozi wa mataifa matatu ya ukanda huo ya Tanzania, Kenya na Uganda kushirikiana kuwakandamiza raia. Amesema hayo alipozungumza na DW.
Amesema anadhani watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wana jukumu la kushikamana ili kuhakikisha wanadhoofisha mielekeo ya kiimla na ukiukwaji wa haki.
Karua alizuiwa kuingia Tanzania mapema wiki hii, alipokuwa akienda kuhudhuria kesi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha CHADEMA, Tundu Lissu, kama mwangalizi. Lissu anakabiliwa na mashitaka ya uhaini na uchochezi.
Kwa sasa Karua anamwakilisha mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye pia anatuhumiwa kwa uhaini.