Marine Le Pen apigwa marufuku kugombea urais wa mwaka 2027
31 Machi 2025Matangazo
Jaji katika kesi hiyo, pia amemhukumu kifungo cha miaka minne jela lakini hatokwenda gerezani, ikiwa ni pamoja na miwili ambayo amehukumiwa kifungo cha nyumbani. Le Pen ametakiwa kulipa faini ya dola 108,200.
Mahakama yaonyesha nia ya kisiasa
Wallerand de Saint-Just, aliyekuwa mweka hazina wa chama cha Le Pen cha National Rally, amesema mahakama hiyo imeonyesha nia yake ya kisiasa, na wala sio ya mahakama na kisheria.
Le Pen kukata rufaa katika uamuzi wa kesi dhidi yake
Kulingana na wakili wake, Le Pen, mwenye umri wa miaka 56, atakata rufaa na kwamba hakuna kifungo cha jela wala faini kitatekelezwa hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa.