Marekani yazingatia azimio jipya la Iraq:
16 Machi 2004Matangazo
WASHINGTON. Marekani inanuiya kuendeleza harakati za wanajeshi wa Kispania nchini Iraq kwa kuhimiza azimio jipya la Umoja wa Mataifa (UM). Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje aliarifu kuwa kufuatana na hatua ya kukabidhiwa madaraka serikali mpya ya mpito ya Iraq hapo mwishoni mwa Juni umezuka uwezekano mpya kuwa Baraza la usalama la UM likapitisha azimio jipya la Iraq. Baada ya ushindi wake wa kushangaza katika uchaguzi wa bunge, Waziri Mkuu mteule wa Uspania José Luis Rodrígues Zapatero amesema ana niya ya kuwarejesha nyumbani wanajeshi 1300 wa Uspania waliyoko Iraq kabla ya Juni 30 ikiwa hawatopata kibali rasmi cha Umoja wa Mataifa cha kubakia huko.