Marekani yawaita raiya zake waihame Saudi Arabia
18 Desemba 2003Matangazo
WASHINGTON: Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imewaita raiya wa Kimarekani nchini Saudi Arabia wachukua hatua kali za tahadhari kufuatana na kitisho cha kuweza kufanyika mashambulio mengine ya kigaidi. Wanadiplomasia wote ambao kuendelea kuweko kwao Saudia hauna umuhimu mkubwa wameitwa kuihama nchi. Nao jamaa wa maafisa wa Kimarekani wameitwa waihame Saudi Arabia. Hata Wamarekani walioko Saudi kwa sababu za kibinafsi wameitwa wazingatie kuondoka nchini humo. Hapo mwezi uliopita wa Novemba waliuawa watu 17 na kujeruhiwa zaidi ya 100 katika shambulio la bomu katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riadh.