SiasaUrusi
Marekani yawafunza wanajeshi wa Ukraine
16 Januari 2023Matangazo
Hatua hiyo inalenga kuwapa mafunzo ili waweze kurejea kwenye uwanja wa mapambano dhidi ya wanajeshi wa Urusi katika kipindi cha wiki tano hadi nane zijazo. Hayo yameleezwa na mwenyekiti wa wakuu wa majeshi ya Marekani Jenerali Mark Milley ambaye anapanga hii leo Jumatatu kutembelea kambi ya Grafenwoehr kujionea mpango huo.Kwa mujibu wa jenerali huyo wanajeshi wa Ukraine wanaoshiriki mafunzo hayo waliondoka Ukraine siku chache zilizopita.Silaha chungunzima na vifaa vingine vimeshaandaliwa kwaajili ya mafunzo hayo nchini Ujerumani. Mafunzo hayo ya kijeshi ya Marekani kwa wanajeshi wa Ukraine yanakuja wakati mapambano makali yanashuhudiwa katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk ambako wanajeshi wa Urusi wanaudhibiti mji wa Soledar.