SiasaMarekani
Vita Ukraine: Marekani kujiondoa kwenye mchakato wa amani?
18 Aprili 2025Matangazo
Rubio ameitoa kauli hiyo mjini Paris baada ya kushiriki siku ya Alhamisi mkutano kati ya maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na mataifa ya Ulaya kuhusu vita vya Ukraine na juhudi zilizokwama za usitishwaji mapigano, zilizoanzishwa na rais Donald Trump.
Soma pia: Ufaransa yasifu mkutano na Marekani juu ya vita vya Ukraine
Mkutano mwengine unatarajiwa wiki ijayo mjini London na Rubio amesema ndio utakaoamua ikiwa Marekani itaendelea kujihusisha na mchakato huo wa amani. Urusi imesema iko tayari kwa mazungumzo lakini kwa kuzingatia maslahi yake. Hayo yanajiri wakati Ukraine na Marekani zikitarajiwa wiki ijayo kusaini mkabata wa madini.