JamiiMarekani
Marekani yatangaza dola milioni 50 kwa atakayemkamata Maduro
8 Agosti 2025Matangazo
Wizara ya Sheria na ya Mambo ya Kigeni zilitangaza kitita hicho kupitia Mwanasheria Mkuu wa serikali Pam Bondi.
Kwenye video iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, Bondi amemshutumu Maduro kushirikiana na makundi maarufu ya uhalifu kama ya Tren de Aragua na Sinaloa.
Utawala wa Trump unamshutumu Maduro kwa kuwa mfanyabiashara mkubwa zaidi wa dawa za kulevya duniani, akishirikiana na makampuni ya biashara kuingiza dawa hizo nchini Marekani.